Tafuta DHWTangazaTuandikie
BLUE IRIS Rangi ya mwaka!!

BLUE IRIS Rangi ya mwaka!!

kwa mujibu wa mtandao wa pantone color institute ambao wanashughulika na rangi imedai kuwa BLUE IRIS ndo rangi ya mwaka huu

Hilo nililithibitisha katika tukio la Grammy Award ambapo masuper staa kibao wamajauu walikuwa wametinga rangi hiyo.

Rangi hiyo si nyengine bali ni blue iliyokolea na ile blue inayoelekea kwenye zambarau nzito

Wajuzi wa mambo wamedai kuwa ndio hiyo rangi nzuri ila itapendeza zaidi kwa nguo za usiku Evening dress sio rangi ya kuvaa masaa yote... Nadhan ustukia hilo ndo maana hajamwaga nyingi mitaani hadi sasa nimeonaviatu ila navyo ni vya mtoko tu

Na wale wenzangu na mie ambao tunapenda kutumia rangi ya mwaka kama rangi za harusi kwa rangi hii tumechemsha... haipendezi kuwa rangi ya harusi...hivyo endeleeni na zile zile apple green, baby Blue nk

Habari ndo iyoooo


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.