Tatiana kukanyaga ardhi ya kandoro leo
Yule mwakilishi kutoka Angola katika shindano la Big Brother Africa II Tatiana Durao, anatarajiwa kukanyaga ardhi ya Tanzania leo majira ya saa nane mchana.
Mshiriki huyo kutoka Angola atakuwa hapa nchini kwa ajili ya mwaliko maalumu, na atafanya maonyesho ya mavazi Arusha Aprili 25 kabla ya kufanya Dar es Salaam siku inayofuata.
Naye Mratibu wa ziara hiyo Petter Mwendapole Durao atawasili kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini.
Pia tiketi kwa ajili ya onyesho hilo tayari zimeshaanza kuuzwa tangu juzi, zikiwemo zile za viti maalumu na kawaida pia.
Pia kwa upande wa onyesho lake la hapa bongo, Durao atasindikizwa na bendi ya Kilimanjaro, ‘Njenje’.
Na kiingilio cha Dar es Salaam kitakuwa Sh 100,000 kwa mtu mmoja huku kikiambatana na chakula cha usiku na kiingilio cha Arusha kitakuwa Sh 50,000.
Pia Washiriki wa shindano la Kisura wa Tanzania pamoja na Mabalozi wa Redd’s, Victoria Martin na Jokate Mwegelo watamsindikiza Durao katika maonyesho yake akiwemo Edna Makanzo, Emmy Mahalu, Irene Shirima, Neshino Laizer pamoja na Vyonne Joseph.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala