Tafuta DHWTangazaTuandikie
fainali ya visura wa Tanzania



Kisura wa Tanzania anatarajiwa kujulikana April 26 katika fainali za shindano hilo ndani ya ukumbi wa hotel ya Moven Pink jijini Dar Es Salaam.

Akiongea Darhotwire mratibu wa shindano hilo Irene Kiwia alisema kuwa warembo hao watapanda jukwaani na kujajiwa na majaji kuwa nani anastahili mkataba.

...Visura waliongia fainali ya tano bora ambao ni Emmy, Edna, Irene, Neshino na Yvvone watapanda jukwaani kuonyesha mavazi yaliyobuniwa na wabunifu wa hapa nyumbani na hapo ndo mshindi atachaguliwa....alisema Irene

Alitaja wabunifu hao kuwa ni Ally Remtulla, Zamda George, Robbi Morro, Napelel Africa na Francissca Shirima. na mmoja kati ya majaji wa siku hiyo ni mshindi wa Big Brother Afrika2 mwanadada kutoka Angola Tatyana Durao

Mshindi wa shidano la kisura atapata mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya O Model Africa ya Afrika ya Kusini wenye thamani ya dola za kimarekani 52,000.00 na ataanza mkataba rasmi mwisho wa mwezi wa Mei

Kila la kheri visura


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.