Miss TZ Canada kusakwa!
Wimbi la kuenea kwa shindano la Miss Tanzania nje ya mipaka ya nchi limezidi kuenea, baada ya Watanzania wanaoishi Canada nao kuamua kuendesha shindano huko, ili mshindi aje kuchuana katika fainali za taifa nchini.
Awali, Watanzania waishio London, England ndiyo waliokuwa wakiendesha shindano nje, lenye hadhi sawa na mashindano ya ngazi za kanda kwa mikoa ya nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano la Miss Tanzania (Canada), Samora Mkandawile, alisema shindano lao litafanyika Juni Saba katika mji wa Toronto.
“Tunatarajia kuwa na washindani 15 na maandalizi yanaendelea vizuri sana. Washiriki ni wasichana wa Kitanzania wanaoishi kule,” alisema Mkandawile.
Kwa nchini, hatua ya awali ya shindano la Miss Tanzania kwa ngazi za vitongoji (Dar es Salaam) na kwingineko, ndiyo zinatarajia kuanza mwezi ujao, kuanzisha mbio za kuwania taji linaloshikiliwa na Richa Adhia, aliyeshinda mwaka jana.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala