supu ya mahindi na vipande vya mbavu za mbuz
Mahitaji
Mhindi mmoja, mbavu za mbuzi gramu 200, tangawizi gramu 5, vitunguu maji gramu 5, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, na chumvi vijiko vitatu.
Njia
1. kata kata mbavu za mbuzi ziwe vipande, kata muhindi uwe vipande vipande, kata kata vitunguu maji na tangawizi.
2. chemsha maji kwenye sufuria halafu tia vipande vya mbavu za mbuzi kwenye sufuria ili kuondoa damu, na kasha vipakue.
3. washa moto, mimina maji kwenye sufuria, tia vipande vya mbavu za mbuzi, vipande vya muhindi, vitunguu maji na tangawizi, halafu mimina mvinyo wa kupikia, baada ya kuchemka, punguza moto, endelea kuchemsha kwa dakika 40, baada ya hapo tia chumvi halafu ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kunywawa.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala