Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni Emmy Milao



Kisura Emmy Milao kutoka Arusha amefanikiwa kuvishwa taji la Kisura wa Tanzania na kufanikiwa kuwabwaga visura wengine wanne

Katika kinyang'anyiro kilichofanyika ndani ya hotel ya Moven Pick Emmy alionekana kuwafunika wenzie katika kunata na stage

Warembo wengine waliofanikiwa kufungua duru la tatu bora ni pamoja ja Edna Makanzo kutoka Dar na Yvvone Ramomi kutoka Zanzibar.

Kwa ushindi huo Emmy amefanikiwa kuzoa mkataba mnono wa milioni 52 wa kufanya kazi na kampuni ya O Model inayomilikiwa na mwanamintindo Oluch yenye makazi yake nchini Afrika ya kusini

Shindano hilo pia lilisindikizwa na mdada kutoka Angola Tatyana a.k.a Wifi ambaye nae alipanda jukwaani kuonyesha kipaji chake cha uanamitindo

Kila la kheri Emmy bila shaka utaipeperusha Bendera vyema ukishirikiana na Hawa Abdul Kadir na Happiness Magesa ambao wanafanya kazi za uanamitindo nchini humo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.