Tafuta DHWTangazaTuandikie
Tuzo za vinara zaiva!!

Zoezi la ukusanyaji wa filamu zitakazoshiriki katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania lilimalizika rasmi ijumaa ya Aprili 18 ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kufanyika kwa shughuli ya utoaji wa tuzo hizi.

Tuzo hizo ambazo zinatolewa na Kampuni ya One Game Promotions ya jijini Dar es Salaam wamefanikiwa kupokea filamu 122 lakini ni filamu 72 ndizo zimefikia kiwango kinachohitajika katika tuzo hizo kwa mwaka 2007/08.

Akiongea na Darhotwire mratibu wa tuzo hizo Khadija Kalili alisema kuwa waigizaji wengi karibia wote wameitikia wito na majaji wana kazi kubwa ya kuchambua kazi zao


...Kukamilika kwa hatua hatua hiyo ya ukusanyaji wa filamu hizo ndio mwanzo wa hatua nyingine katika kuelekea kupatikana kwa wasanii watakaofanikiwa kutwaa tuzo hizo kwa mwaka huu....

Jopo la majaji litazipitia filamu zilizoingia katika tuzo na kuibuka na majina matano katika kila kipengele na baadae kusubiri hadi siku ya onyesho ya kutolewa kwa tuzo hizo kwa ajili ya kutambua atakayeibuka na tuzo katika kila kipengele.

Siku hiyo zitatolewa tuzo ishirini pamoja na tuzo ya heshima kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa kwa sanaa ya uigizaji nchini. Hivyo kutakuwa na vipengele 19 zitakazokuwa na majina matano ambapo mmoja wao atatwaa tuzo.


Utoaji wa tuzo hizo linatarajiwa kufanyika Mei 30 mwaka huu.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.