Pale za comedy wanapotoa 'chorus'
Vijimsema kibao pamoja na vitendo vya kundi la Ze comedy vimeenea mitaani kama sio Bongo nzima kiasi cha kupelekea kmakundi mbalimbali ya muziki nchini kupata cha kuimba au kunogeshea miziki yao
Hayo nimeyathibitisha kupitia nyimbo ya mama wa mipasho maarufu jijini kama Khadija Kopa katika wimbo wake mpya wa Why?!!
Katika wimbo huo kuna kiitikio kinasema Why?!!...kwanini...endeleaaaa...Hayo yakiwa ni maneno ambayo yanapendwa kusemwa na mchekeshaji Mac Regan
Kama hiyo haitoshi nalo kundi la Jahazi Modern Taarab wana nakshi nakshi wana kichombezo chao katika sebene zao kinachosema...cheza kijot jot na kushtua...huku style ya kucheza ikiwa ni ile ya mwendo atembeao Jotti katika michezo yao ya kila alhamis ndani ya Runinga ya EATV
Ukiachia mbali misemo kama Mdebwedo, kugandamiza, mwanawane, namengine kibao imeenea mitaani ambayo hutoka katika vinywa vya wachekeshaji hao.
Na huo ni mwanzo!!

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala