Tafuta DHWTangazaTuandikie
Dar City Centre June 14

Shindano kumsaka miss Dar City Centre linatazamiwa kufanyika Juni 14, jijini Dar es salaam.



Mratibu wa shindano hilo Dennis Ssebo alisema shindano hilo linatazamiwa kushirikisha warembo wapatao 15.

Ssebo alisema lengo la shindano hilo nikutafuta mrembo atakaye weza kufikia vigezo vya kimataifa .

Aliwataka wa rembo kujitokeza kwa wingi kutokana na shindano hilo kuwa na zawadi bomba kuliko vitongoji vingine.

Ssebo alisema anatazamiwa kukutana na waandishi wa habari may 14, ambapo ndio atatangaza zawadi za shindano hilo, wadhamini na wasanii watakao burudisha siku hiyo.

Kambi ya washiriki wa shindano la miss Dar Cinty Centre inatazamiwa kuaza may 14 katika ukumbi wa Cine Club, jijini Dar es salaam.

Ssebo alisema wataaza mazoezi chini ya aliyetwaa taji hilo mwaka jana Latifa Warioba na mrembo mwengine shubi.

Ssebo alisema tayari fomu za wle wanaopenda kushiriki katika shindano hilo zimeshaanza kutolewa .

Alieleza fomu hizo zinapatikana Shear lllusion, Golden Touch Sloon, Millenium Towers, Fabak Fashion, Regency Park hotel na Easy Finance.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.