Jitokezeni Miss Sinza
Waandaaji wa shindano la urembo la Miss Sinza...wametoa wito kwa vidosho warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji hicho.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu alisema kuwa kitongoji hicho bado kinatoa nafasi kwa warembo walio na sifa kujaribu bahati zao.
“Kuna warembo wachache ambao wamejitokeza mpaka sasa huku tayari waliwasili wakiendelea kujifua kila siku kwenye ukumbi wa Vatican City, Sinza kuanzia saa 10 jioni."
Nafasi bado zipo na mrembo mwenye nia ya kushiriki anatakiwa kufika katika ukumbi huo,” alisema.
“Kitongoji cha Sinza kina historia nzuri katika mashindano ya urembo hivyo tunawahimiza wajitokeze maana mwaka huu tunatarajia kutoa zawadi nzuri na kubwa,” alisema.
Shindano la kitongoji cha Sinza limepangwa kufanyika mwezi June katika tarehe itakayotangazwa hapo baadae.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala