Tafuta DHWTangazaTuandikie
Jopo la majaji kumalizika Mei 17

Tangu jopo la majaji lianze kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa na watayarishaji wa filamu hapa nchini, ili kuwania tuzo za Vinara (Vinara Film Award) sasa yapata kama wiki moja sasa na kumeweza kuwa na ushindani mkali miongoni mwa filamu hizo.




Mchuano huo umetokana na sehemu kubwa ya filamu hizo kuweza kuwa na kiwango cha hali ya juu na ubora zaidi.

Kazi ya kupitia filamu zilizowasilishwa inaendelea vizuri na kazi hiyo itamalizika kwa wakati uliopangwa, kwani filamu na wasanii vinachuana makoo kwa viwango vya juu.

Pia Majaji hao wanatarajiwa kumaliza kazi hiyo Mei 17 ndani ya mwaka huu na itatangaza majina matano kwa tuzo zipatazo kumi na tisa zitakazowaniwa.

Onesho hilo la utoaji tuzo linatarajia kufanyika Mei 30 ndani ya mwaka huu, kwani wiki chache zilizopita filamu sabini za kibongo zimewasilishwa na watengenezaji wa filamu wa hapa nchini kwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka 2007/08.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.