Tafuta DHWTangazaTuandikie
M's Dar Indian Ocean yanukia

Warembo 10 wamerudisha fomu za kushiriki shindano la kumsaka Miss Dar Indian Ocean 2008, litakalofanyika hapo baadaye.



Naye Mkurugenzi wa Jacques Collections Jackline Mafuru alisema kuwa warembo hao wamesharejesha, fomu za ushiriki na kuwa tarehe kamili ya shindano hilo itatangazwa hapo baadaye.

Mafuru alisema bado kampuni yake inakaribisha warembo wenye sifa, ili waweze kujitokeza na kushiriki.

Alisema majina ya warembo, mazoezi, mwalimu wa mafunzo, zawadi, ukumbi wa mashindano pamoja na tarehe ya mashindano vyote vitatangazwa hapo baadaye.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba wadau wa mashindano ya urembo wanajua historia ya Miss Dar Indian Ocean, ndani ya Miss Kinondoni na Miss Tanzania hasa baada ya ushindi wa Nancy Sumari na Natalia Noel mwaka 2005.

Alisema kwa kusema kwamba ikumbukwe kuwa Nancy (Sumari) alikuwa mshindi wa pili wa kitongoji hiki, na katika Miss Kinondoni na Tanzania akashinda nafasi za kwanza, Wema Sepetu Miss Tanzania 2006 naye alitokea hapo hapo.


Kwani Richa Adhia na Lilian ndiyo washindi wetu wa mwaka jana, na hapa ndipo ulipo mtambo wa kutoa warembo bora wa mashindano ya Miss Tanzania.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.