Flaviana aanza kula matunda!!
Mwanamitindo wa Kitanzania anayeibukia kwa kasi kwenye fani hiyo Falviana Matata amezidi kulamba bingo baada ya kualikwa nchini Japan kwa mwaliko wa kampuni ya magari Wilna International.
Flaviana aliondoka Tanzania mwezi mmoja na nusu uliopita na sasa nyota yake inaonekana kungara zaidi baada ya kupata zali hilo ndani ya muda mfupi tu aliokaa Afrika Kusini.
Akiwa huko Flaviana amepata Junes Modeling Agency iliyoko Ropongi Nishi Azabu ambao atafanya nao kazi na ikiwezekana anaweza hamishia makazi nchini humo
Itakumbukwa Falviana alkuwa mshiriki wa kwanza kwa watanzania kwenye shindano la ulimbwende la ulimwengu yaani Miss Universe ambapo alifanikiwa kuishika dunia.
Kila la kheri Flaviana

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala