Asia Idarous mbunifu mkongwe
Anasema alianza sanaa kwa mwaka 1986, ile ya kiprofetional,lakini kabla ya hapo alianza mwaka 1981 ambapo alikuwa miaka 14 akiwa na hamasa ya kujua kushona ndipo wazazi walipoona wasimbanie na wampe nafasi na nafasi akaitumia na hata hadi leo anahesabu ameshafanya fashion show 75 tangu ameanza
Namzungumzia Mbunifu mkongwe wa mitindo nchini Asia Idarous ambaye ni mama Mlezi wa Tanzania mitindo House ambaye alizaliwa kisiwani Zanzibar na kupatiwa elimu huko ambako alisoma hadi kidato cha nne kabla ya kuingia chuo cha uchumi.
Akiwa na miaka 14 ndipo wazazi walimpeleka chuo cha kujifunza kushona mwenyewe anakiita 'Cutting class' ambako alikuwa anajifunza kukata na kushona nguo.
"Kutokana na hamasa niliyokuwa nayo ya ubunifu wazazi wangu walinipeleka shule kusomea kushona ambako iliniwezesha mimi kuweza kukata na kuweza kushona"alisema Asia
Nilitaka kujua je huko kwao kuna mtu alikuwa na hichi kipaji au
mie hii ilikuja baada ya kuwa napenda saana kuvaa, sasa nikawa naona yanini kugombana na mafundi au hata waniharibie vitambaa na mshono wangu ndipo nilipoamua kwenda kusomea kushona.
Alisema alishafanya maonesho ya mavazi 75 nje na ndani ya nchi
Na kisa hasa hadi nikaenda shule ni baada ya kupeleka kitambaa kwa fundi nikakuta bado hajashona namie nguo naitaka ndo nikaona bora nikajifunze niepukane na mafundi alitanabaisha Asia
mwaka 1986 Asia alienda nchini Uingereza ambako alisoma hasaa Diploma ya ubunifu wa mavazi katika Chuo cha KAYS na mwana huo huo aliporudi ndipo alifanya fashions show yake ya kwanza jijini Mwanza akiwa amealikwa na Mama wa Kigoha aliyekuja kufanya show na kuambiwa kuna mbunifu pale hotelini, wakati huo Asia akiwa Mwanza kikazi akiwa ameambatana na mumewe aliyekuwa meneja wahotel
Katika Show hiyo Asia alifanikiwa kuuza nguo alizozibuni ndipo akaona kumbe show zinalipa ndipo nae akaandaa show yake mwenyewe ambako alionesha nguo 28 tu, na ilifanikiwa saana.
Akielezea historia yake kiubuifu Asia anasema 1987 alifanya fashion show iliyombatana na shindano la Miss Victoria ambako Shyrose Banji ndie aliyeshinda katika shindano hilo.
Baada ya kufanikiwa ndo nikawa nafanya show mara kwa mara na katika moki tofauti ikiwepo Moshi, Arusha, Zanzabar na Dar es salaam Ukizingatia mume wangu alikuwa hoteleya hivyo tulikuwa tunaenda kikati mahoteli tofauti.
Kwa sasa show ninayofanya mie mwenyewe kuiandaa ni Lady in Red show ambayo nafanyaga kabla ya valentine day na Kanga za kale show ambayo naonesha mavazi mbalimbali ya kanga
Nje ya nchi Asia alishafanya show nchini Nairobi kwenye Safari Carnival na Abudhabi Fashion Week na German ambako nadesign nguo napeleka inafanyika kwenye fashion show zao katika sekta ya kuonesha mavazi toka Afrika
Asia anazo tuzo alizotunukiwa ni Smilling Face,Safari Fashions Carnival na Miss Mirinda.
Nilitaka kujua Asia analitambuaje vazila taifa yeye kama mbunifu
"kwa kweli mie naona vazi la taifa ni kanga....sasa mtu utalishonaje na tungependekeza mtu akivaa kanga awe na kabendera ya taifa au itengenezwa kibendera maalum kwenye kanga ambapo mtu akiona anajua hii ni ya Tanzania
Kama kilivyo kitenge kile toka nchini Ghana kinavyotambulika ni cha nchi gani.
Asia anasema mbali na kuwa mbunifu yeye ni mrembaji pia "Beautician" ambapo anaweza mremb biharusi au yeyote anayetaka kurembwa kuanzia kusingwa hadi kuwekwa make up
Nilitaka kujua Role Model wa Asia
...Ah ni mimi mwenyewe...kama nilivyokwambia mie ubunifu sikuiga wala kurithi kwa yeyote ni kitu nilizaliwa nacho.
Darhotwire inamtakiwa kheri na mafanikio katika kazi za mikono yake azifanyazo kila ziku.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala