Tetesi zimezagaa
mastaa wa filam Tanzania wamedhulumiwa haki yao na kampuni moja inayojulikana kwa jina la Billionaire Club(Escape)
Kwa mujibu wa mtandao wa Ray Kampuni hiyo iliwaahidi mastaa hao kuwalipa malipo mazuri na ahadi kemkem kwa minajili ya kufanya nao kazi za kutengeneza filam na Tamthilia kwa kuingia nao mikataba ya miezi sita ,badala yake wasanii hao walifaidi mkataba wao kwa muda wa mwezi mmoja na baada ya hapo hali ikawa tofauti na mkataba unavyosema na wamiliki wa kampuni hiyo kuanza kuwakimbia wasanii hao.
Sakata hili limeibuka baada ya msanii Vanita Omary ambaye anajishughulisha na make up na costume kupelekwa polisi na mmoja wa mabosi wa kampuni hiyo baada ya kukataa kurudisha costume za kampuni hiyo mpaka watakapolipwa haki zao ndio warudishe
Wasanii ambao wako kwenye mkumbo huo ni Yusuph Mlela,Monalisa,Thea,Big Matovolwa,Rose Ndauka,Vanita Omary,Frank Mwikongi
Kipindi cha Bongo Movie kimeteta nao...tusubiri luningani EATV .

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala