Lady in Red yafana
Mwishoni mwa wiki ndipo lilipofanyika onesho la mavazi ambalo limefanyika kwa mwaka wa tano sasa la Lady in Red ndani ya ukumbi wa hotel ya Kempysik.
Mwanadada Elizabeth Gupta aliyetuwakilisha katika shindano la Big Brother mwaka jana ndiye aliyefungua pazia akiwa ndo Lady In red mwenyewe.
kisha Warembo walianza kuonesha nguo za wabunifu waalikwa kabla ya kuja Mama Lao Asia Idarous na kuonesha mavazi yake.
Wadau walijitokeza kwa wingi huku Bendi ya Machozi Band ikiwa inatumbuiza na kikundi cha Simba kikichombeza kwa burudani.
waliofanikiwa kupata tuzo za mbunifu bora wa mwaka ni Farha na tuzo ya Beauty with Purpose ilienda kwa Elizabeth Gupta.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala