Share |

Chapati na Nyama ya Mbuzi

Chapati hizi ni safi kabisa kwa Familia kubwa kutopika mara kwa mara unapika nyingi na unazitunza wiki moja na zikabaki na ubora uleule, pia Nyama hii ya Mbuzi inakua haina harufu...mtu yeyote anaweza kula kwa aina hiyo ya mapishi na akafurahia sana.
mahitaji: 

1 kg unga wa ngano
1 kikombe kimoja
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
nusu kikombeha chai mafuta ya kupikia
2 mayai kuongeza ladha

JINSI YA KUANDAA

-Unga wa ngano
-Weka mafuta katika unga
-Kisha weka moto sana katika unga
-Kisha changanya kwa kutumia mwiko maana maji ni yamoto sana
-Weka chumvi
-Kishaanza kukanda kwa mkono maji yatakua yameshapoa
-Kanda unga safi kabisa uchanganyike
-Kisha anza kusukuma unga wote
-Baada ya hapo mwagia kwa juu mafuta ya kula pakaza eneo lote
-Hakikisha mafuta yameenea unga wote
-Kisha geuza a upande wa pili paka pia mafuta
-Toa weka katika sahani itakua imeiva safi kabisa tayari wa kuliwa
-Weka pembeni zipoe kisha unaziwekakatika sahani unatumbukiza katik mfuko wa plastiki usiweke kwenye friji weka tu nje zitakua safi na laini zinakaa wiki 1 baada ya hapo zitapoteza ubora ukitaka kula unatoa unapasha kwenye kikaango au kwenye micro wave inakua yamoto na laini zaidi na iliyochambuka kwa ubora uleule

MAHITAJI NYAMA YA MBUZI

1 kilo nyama ya mbuzi
1 kitunguu kikubwa
1 nyanya ya kopo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu
3 viazi ulaya
1 kikombe kilichojaa mchanganyiko w mboga majani
1 kikombe cha maji baridi
1/2 kikombe mafuta ya kupikia

-Weka mafuta katika sufuri yakishapata moto weka kitunguu maji kaanga
-Kaanaga vitunguu mpaka viwe vya kahawia ili kuleta ladha nzuri katika mchuzi wako na kuondoa harufu ya mbuzi ili mtu yeyote yule aweze kula
-Baada ya kitunguu kuwa kahawia weka nyama ya mbuzi piaendkea kukaanga
-Ongeza maji kiasi ili sufuria isiungue pamoja na nyama
-Kisha weka chumvi
-Acha mbuzi ichemke na itakua na mchuzi wa kahawia
-Kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kusagia kitunguu swaumu
-Baada yahapo weka viazi uklaya vilivyomenywa safi na kukatwa katwa vidogo
-Kisha weka nyanya ya kopo
-Kisha weka mchanganyiko wa mboga majani ( caroti, njegere na pili pili hoho, mahindi machanga ya njano)
-Kuongeza ladha zaidi unaweza weka unga wa binzali au rojo la binzali

Kwa hisani ya Issa Kesu