Share |

Mkate wa mayai na jam

mahitaji: 

Mahitaji
Boflo kubwa 1
Mayai 4
Samli 1/4kg
Unga wa ngano kiasi

Namna ya kutengeneza

Kata mkate vipande vyembamba uvipake jam, kisha vigandishe kimoja juu kingine
Vunja mayai yapige sana.

Kisha nyunyiza unga huku ukiendelea kupiga mayai
Injika chuma cha chapatti ( frying pan) utie samli ikianza kuchemka, chovya mikate iliyogandishwa katika mchanganyiko wa mayai na ngano na ukaange ndani ya chuma, ikiwiva geuza upande wa pili.

Ikiwiva yaani ikiwa na rangi ya kahawia, vitoe na uvitie kwenye sahani. Tayari kwa kuliwa.

Kwa hisani ya  Maimuna Kubegeya