1/2 Unga wa ngano
1 kilo nyama ya kusaga
1/2 kilo ya kitunguu
1 carroti
1 pili pili hoho
1/2 maji baridi
1/2 kijiko cha chai chumvi
1/Kata kitunguu,pili pili hoho na carroti kwa vipande vidogo.
2/Kaanga vitunguu vikisha iva weka pembeni.
3/Kaanga nyama ya kusaga kisha weka chumvi ili iive na nyama mpaka ikauke maji yote ili samosa iwe na ladha nzuri.
4/Kisha weka karoti baada ya nyama kukauka vizuri.
5/Kisha weka pili pili hoho.
6/Kisha weka vile vitungu vilivyokwisha kaangwa mchanganyiko utakua safi.
7/ Kisha weka kitunguu swaumu kaanga kiasi na chukua mchanganyiko huu weka pembeni upoe ili nyama na manda visiharibike
8/Chukua unga nusu kilo weka maji nusu kikombe.
9/Kanda mchanganyiko wa maji na unga mpaka uwe ngumu ikiwa laini itakatika katika
10/Sukuma mduara mdogo kisha paka mafuta ya kula juu yake.
11/Mwagia unga kiasi kuzunguka mduara wote kusaidia manda zisishikane baada ya kuchomwa.
12/Kumbuka kusukuma kisha paka mafuta halafu nyunyizia unga kisha zipandanishe kwa juu mpaka zifike miduara 5 zitatoa samosa 20.
13/Kisha usukume mduara huo wenye samosa 5 mpaka upate chapati moja nene na pana usawa
wa kikaango chako
14/Choma katika kikaango kwa moto wa wastani ili usiunguze choma dakika 2 kila upande kisha
geuze
15/Kisha toa ikiwa ya moto anza kuzibandua kwa haraka kabla hazijapoa moja baada ya nyingine
16/Kisha kata kati kwa kati pande nne kwa usawa
17/Kisha kata kuzunguka manda hiyo ili kuweka mzunguko sawa
18/Kisha chukua unga kiasi na maji changanya iwe nzito itatumika kama gundi angalia picha jinsi
gundi ilivyopakwa kwa juu
19/Kisha kunja upande wa kuli hakikisha unaandamiza ili gundi ikamate
20/Kisha kunja upande wa kushoto kandamiza pia ili gundi ishike
21/Chukua kijiko kisha weka nyama katika manda yako
22/Paka gundi kwa juu kisha funga manda yako
23/Choma katika mafuta yenye moto wa wastani ili zisiungue na ziwe kaukau
24/Samosa zkiwa katika moto kumbuka kuzigeuza mara kwa marazisiungue upande mmoja
Nusu kilo ya nyama yakusaga inatoa samosa 40 - 50 kwa matumizi ya nyumbani
Kwa biashara nusu kilo ya nyama ya kusaga na kilo ya vitunguu, karoti 5 napili pili hoho 5 unapata samosa 100
Maandalizi sio magumu sana ila samosa huwa inauzwa ghali sana kokote duniani
