Ziara za Mawaziri ni kitendawili
Mawaziri na Manaibu wamefanya katika ziara mikoa mbalibali wanayodai ni kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya 2007/2008.
Mawaziri wamechukua zaidi ya wiki moja katika ziara yao wakiongea na wananchi wao kupitia mikutano ya hadhara kuwaelezea mipango mbalimbali iliyomo katika bajeti hiyo.
Ziara hiyo ya mawaziri wote wa serikali ya awamu ya nne imezua mjadala miongoni mwa wananchi ikiwa imepita tangu bajeti hiyo isomwe bungeni na waziri wa Fedha Zakia Meghji.
Wapo baadhi ya watu wanadhani kuwa ziara haina kitu kipya zaidi itakuwa ni kutumia vibaya fedha za walipa kodi kwa sababu kitu wanachokwenda kukielezea hakistahili kutumia kiasi hicho cha fedha na muda.
Wapo wananchi wanadani kuwa ziara hiyo haistailikitu ambacho wako sahihi kabisa tunaungana na watu hao kueleza kufanya ziara kwa ajili ya kuwaeleza wananchi mipango iliyomo katika bajeti ni kazi ambayo ni ya kiutendaji zaidi.
Ni vyema ziara kama hiyo ingefanywa muda mfupi mara baada ya kusomwa bajeti hiyo watu wangeweza kuelewa ujumbe ambao kuliko sasa hivi.
Ziara kama hiyo ni gharama kubwa kwa sababu mawaziri hao sio kwamba wapo peke yao bali wameambatana na watu wengine na wote wanalipwa fedha za walipa kodi
Vile vile, tukumbuke kwamba tangu bajeti hiyo isomwe bungeni viongozi mbalimbali wa kitaifa wamefanya ziara nyingi mno katika mikoa hiyo pamoja na mambo mengine walielezea utekelezaji wa bajeti hiyo.
Lakini pia tunakumbuka kwamba serikali imekuwa ikifanya semina elekezi mbalimbali viongozi wake kuanzia makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya, na wakurugenzi wa halmashauri kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kutekeleza majukumu.
Tunachohoji hapa ni nini kimeifanya serikali ghafla kukurupuka kuwatuma mawaziri wake kwenda mikoani kufanya kazi ambayo imefanywa na viongozi wengine wa serikali?
Ni wazi ziara hii ya mawaziri bado inaibua maswali mengi kuliko majibu. Ni vyema sasa serikali pamoja na kuwa na nia nzuri ya viongozi wake kuwatembelea mara kwa mara wananchi ikaanza kuangalia ziara zipi zina manufaa na zipi ambazo hazisaidii.
Kuendelea kutuma mawaziri kufanya ziara ya kueleza utekelezaji wa bajeti kazi ambayo ingeweza kufanywa na wabunge majimboni ni kutoa picha mbaya kwa wananchi kuhusu fedha zao.
Mwananchi.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala