Wizi wa LAPTOP katikati ya jiji!
Kumekuwa na Wimbi kubwa la wizi wa Laptop maeneo ya Jiji la Dar es salaam kwa siku za karibuni haswa maeneo ya Posta Mtaa wa Samora Kwa kutumia Gari Ndogo za kubebea Abiria Taxi , Hii imekuwa Rahisi kwao kwa sababu begi nyingi za Laptop zinajulikana kwa maumbo na Lebo zilizoko kwenye Mabegi hayo .
Mara nyingi inawakuta watu wanaobeba mabegi hayo mikononi , ghafla gari hiyo inaweza kuja kwa nyuma kukutishia kukugonga Ndio hapo Unaporwa Begi Hilo .
Ingawa Tatizo hili limekwepo kwa kipindi kidogo kwa baadhi ya maeneo , hii tabia imerudi tena kwa kasi ya ajabu kwahiyo mnavyotembea huko mitaa kati kati ya Jiji haswa Samora muwe makini sana .
Hata hivyo Laptop nyingi huwa zinauzwa maeneo ya SAMORA Pembani mwa Duka La Kuuza Vitabu , JAMHURI , MKWEPU , FIRE ,NKURUMAH NA KUNA BAADHI YA MADUKA YA VIFAA VYA KOMPUTA HUWA YANASHIRIKI BIASHARA HII KWA KUNUNUA BIDHAA HIZO
NOTE : HAYO MAELEZO YA MAENEO SIO LAZIMA UKUTE VIFAA VYAKO NI KWA TAARIFA TU

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala