Mkubwa aumbuka!
Hawa jamaa utapeli wao ni hivi,wao wanaorodha ya shule zote za mikoani.na wanakuwa watanashati sana kiasi kwamba huwezi kabisa kudhani kama ni matapeli.na mkononi huwa wanashika funguo za gari.
Ilikuwa kama majira ya saa tisa alasiri ijumaa moja natoka zangu mitaa ya IFM(chuo cha usimamizi wa fedha)wakati napita mtaa mmoja karibu na city garden namuona jamaa mmoja amependezeza ajabu.amevalia suruali safi na amekandamizia tai,na kiatu safi.kama mbabaikaji wa mavazi basi haraka ungefikiria kuwa atakuwa afisa flani.
Akanisimamisha,akanisalimia kwa furaha kama mtu anayenifahamu,"mambo?unanikumbuka"nikamjibu hapana,akanitwanga swali kwani wewe "A" level umesoma wapi?nikamjibu Iringa, tosamanganga secondary 1989.Akacheka sana kanakwamba ananifahamu vizuri.akasema"unaona sasa mi nakukumbuka, mimi nilikuwa na kaa pale kwenye kota za shule,na head master wa mwaka ule alikuwa ni kaka yangu,nawakumbuka wanafunzi wengi isipokuwa wengi wenu majina siwakumbuki kwa kuwa ni muda na mlikuwa wadogo sana".wakati huo wote akiongea mimi hata simkumbuki,wala sura yake hainipi kabisa.akaniuliza unafanya wapi sasa kazi?nikamjibu ndiyo nimemaliza chuo cha ualimu natafuta kazi kaka.
Akiwa anaongea maneno mengi bila kunipa nafasi ya kuuliza kama amemeza cd ya bongo fleva,akasema tena "yule head master wa mwaka ule ambaye ni kaka yangu yupo hapa dar es salaam sasa amefungua shule yake tegeta,nitakupatia no yake".anaweza akakupa kazi ya kufundisha kwenye shule yake.
Mpaka pale mi nilishajua kuwa mkubwa alikuwa ananiandaa kunitapeli bila kujua mi nimezaliwa kariakoo mtaa wa likoma.nina ujua utapeli mwingi tu.akaniambia sasa leta sh ,elfu tano tuchukue vocha hapo tumtafute huyo headmaster.wakati nasubiri jamaa anamalizia kuosha gari yangu hapo nyuma.
Ah!! nikamjibu kumbukumbu zangu zinaonyesha kabisa kuwa mwaka ule ambao mimi nimesoma tosamanganga secondary head master alikuwa ni mzungu tena mholand akijulikana kwa jina la sir,IVAN!!!! na hakuwa na ndugu yeyote wala mke.
Na sasa hivi yupo hapa dar ameachana na mambo ya kufundisha,na hapa unavyoniona nimetoka ofisini kwake hapo jengo la kitega uchumi. mbona wewe unavyoongea naona kabisa lafudhi yako ni ya kichaga!!inakuaje mchaga wa kishumondo na mzungu tena mholand?mkubwa acha apate aibu,hata hakuweza kunitazama usoni tena .jasho linamfumuka kama amemeza kaa la moto.
Ikabidi nimchane(nimwambie) tu kuwa "mkubwa tafuta wengine wa kuwatapeli mi nimezaliwa hapo kariakoo mtaa wa likoma na ninafahamu utapeli wa aina tofauti zaidi ya mia tano,da!!! jamaa akasema basi kaka hii siri yako, nimekosea channel.hata kama una mia niachie tu.
Tuliyozoe jiji tunajua ngoma droo nikazama mfukoni nikatoa mia nikampa,nikamwambia nenda kapate mihogo hapo feri kaka mi sitapeliki, kirahisi.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala